Madaktari Wanasema Kwa Kawaida shingo hutakiwa kuwa na vifupa 7 vinavyounda uti wa mgongo lakini kijana mmoja wa kichina mwenye umri wa miaka 15 ana vifupa 10, Kijana huyo alipokuwa na miaka 10 aligundulika akiwa na ugonjwa wa Congenital Scoliosis na alikuwa na kifua chenye umbo lisilo la kawaida hali iliyosababisha awe na shingo yenye urefu wa inch 3 zaidi.
Hali hii ilimpelekea kupata maumivu makali yaliyofanya iwe vigumu kwake kutembea, Ugonjwa wa Congenital Scoliosis unasababishwa na kuongezeka kwa vifupa vya uti wa mgongo wakati wa ujauzito.
“Mara zote yeye husababisha matatizo anapokuwa nje, vifupa vya uti wa mgongo hukandamiza mishipa yake ya fahamu na hali hiyo inasababisha iwe vigumu kwake kutembea” alisema baba wa mtoto huyo Genyou.
Bahati ilikuwa nzuri kwa kijana huyo kwasababu taarifa zake ziliwekwa hadharani na taasisi ya kutoa misaada ya Beijing ilikubali kugharamia matibabu ya kijana huyo na atafanyiwa operation ya kurekebisha uti wake wa mgongo ambayo bila shaka itapunguza urefu wa shingo yake na kumpatia unafuu.