Mvutano na malumbano baina ya wajumbe kuhusu suala la kuzingatia jinsia katika nafasi ya mwenyekiti na makamu wake vimetawala bungeni kufuatia wajumbe wanawake kutaka nafasi hiyo izingatie jinsia huku wanaume wakidai sheria ifuatwe.
Malumbano hayo yameibuka wakati wajumbe wa bunge hilo wakipitia rasimu ya kanuni za bunge maalum la katiba sehemu ya tatu inayohusu mkutano na vikao maalum vya bunge ambapo kanuni ya nane ya sehemu hiyo fasili ya kwanza inayoelezea uchaguzi wa mwenyekiti bunge hilo na makamu wake ambao kwa mujibu wa sheria ya mabaliko ya katiba nafasi hizo zinapaswa zizingatie pande mbili za tanganyika na Zanzibar
Kufuatia malumbano hayo ikamlazimu mwenyekiti wa bunge hilo pandu ameir kificho kutoa ufafanuzi kuhusu upatikanaji wa nafasi hiyo huku akisisitiza uzingatiwaji wa sheria inavyoelekeza .