Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawiliwamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.
“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.
Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.
Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.