
Katika mwaka wa fedha wa 2013/14 serikali imetenga Shilingi bilioni 1 kwa ajili ya chanjo ya homa ya ini pamoja na huduma za uzazi wa mpango, kiwango ambacho kinatajwa kutokidhi mahitaji ya huduma hizo.
Hali hiyo inawafanya wadau wa uzazi wa mpango kuamini kuwa Serikali bado haijaweka kipaumbele kwa suala hilo, wakati nchi iko kwenye tishio la kuwa na ongezeko kubwa la watu ambapo Takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), zinaonyesha kuwa watu milioni 2.7 huongezeka kila mwaka.
Miongoni mwa Wadau hao ni pamoja na Shirika lisilo la kiserikali la Marie Stopes Tanzania ambalo linadai kuwa mbali na ongezeko hilo pia kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa ongezeko la vifo vya akina mama na watoto vitokanavyo na uzazi kama anavyofafanua mkuu wa kitengo cha mawasiliano maries topes Tanzania JOHNBOSCO BASSO.
Katika juhudi za kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na njia za uzazi wa mpango Shirika la Maries Stopes linaendesha mafunzo kwa baadhi ya Washiriki wa Miss Chang’ombe, Temeke, Jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa mwaka 2010 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha
kuwa karibu wanawake 20 hufariki kila siku kwa matatizo ya uzazi ambapo Kutokana na hali hiyo nchi imejiwekea malengo ya kupunguza kiwango cha vifo kutoka vifo 454 kwa kila wanawake 100,000 hadi 193 ifikapo mwaka 2015.
