
Wabunge katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamemchagua Meya wa mji mkuu Bangui, Catherine Samba-Panza, kama Rais wa mpito.
Samba-Panza, ndie mwanamke wa kwanza kuwahi kushikili wadhifa huo..,
Wagombea wanane waliwania wadhifa huo wadhifa aliokuwa anaushikilia Michael Djotodia, aliyeng’atuka mapema mwezi huu kufuatia shinikizo kutoka kwa viongozi wa mataifa jirani.
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa takriban watu hamsini wameuawa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo mwishoni mwa wiki…,
Mapigano yalianza wakati Djotodia alipochukua mamlaka mwaka jana kwa njia ya mapinduzi akiungwa mkono na waasi wa kiisilamu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya waumini wa kikristo.
