Meriam alihukumiwa akiwa mjamzito na kujifungulia gerezani
Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu
Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.