Mwanamke Mmoja Wa Kinaijeria Omolara Irurhe mwenye umri wa miaka 60 amepata mtotowake wa kwanza baada ya kuhangaika kupata mtoto kwa zaidi ya miaka 30 Mama Huyo Amejifungu Mtoto wake wa kike siku ya juma tatu june 16 huko Lagos
Taarifa zinasema Mwanamke Huyo Aliyekuwa Ndoani kwatakribani miaka 31 Na Amekuwa Akijaribu kila njia hasa matibabu ya kihospitali na kuweka imani dhabiti kwa Mungu Wake Jambo Lililomfanya leo kupata matunda haya Anasema imani thabiti kwa mungu, jitihada za matibabu Subira na bila kukata tamaa ndio matokea yake haya leo Mume wa mwanamke Huyo
Mr Adekunle Irurhe Anasema kipindi cha mwanzo alipata Presha kubwa sana ya kutaka kuoa mke mwingine ili apate mtoto lakini baada ya mke wake kuonyesha imani ya matibabu mume huyo aliamua kukata shauri na kumsikiliza mke wake huku akimsupport kwa kiasi kikubwa
Mwanamke Huyo Anakuwa Mwanamke Wa kwanza Africa mwenye Umri Mkubwa Kupata Mtoto kwa njia ya Invitro Fertilization