
Harnaam Kaur
mwanamke mwenye umri wa miaka 23 anayeishi katika mji wa Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza amepokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu asiowafahamu kwenye mitandao kwa sababu ya ndevu zake nyingi zinazomfanya asitofautishwe kirahisi na mwanaume.
Mwanamke huyo ambaye anakabiliwa na tatizo la kuwa na vinyweleo vingi kupita kiasi, tatizo linalojulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary syndrome’, ameeleza kuwa alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa miaka 11 na kwamba alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.
Nukuu: Anajitamba
“Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo pia. Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa hivi.” Amesema Harnaam.
