Hii Kutoka Burundi, Bi Lydia Nsekera ametengeneza Historia Ijumaa iliyopita baada ya kuchaguliwa kuwa Mwanamke wa Kwanza kuwa Mjumbe Wa Kudumu Katika Kamati Ya Utendaji Ya FIFA Kuwa Awamu Yote.
Nsekera amechaguliwa kuwepo kwenye kamati hio kwa muda wa miaka 4 Na Atafanyia Kazi zake Mauritius.
Wakati huo wanawake wengi wawili Moya Dodd kutoka Australia Na Sonia Bien-Aime kutoka Turks Na Visiwa Vya Caicos Wamepewa Awamu Ya Mwaka Moja Kwa Kila Mtu.
Nsekera alishawahi kuwa mwanamke wa kwanza kupewa kazi hio kwa mwaka mmoja tu na sasa amechaguliwa kwa miaka minne.
Kwa sasa patakuwa na wanawake watatu kwenye kamati hio tofauti na miaka miwili iliyopita hapakuwa na hata moja.
Hii imeonekana kama hatua nyingine kubwa ya Usawa Wa Kijinsia Unaofanyika na FIFA. Ila kazi bado kwani kamati ina watu 24 na wanawake ni watatu tu. Imechukua miaka 109 kufikia hapa alisema Rais wa FIFA Sepp Blatter.