
Madona kwa sasa yupo ziarani nchini Malawi akiwa na company ya watoto wake wawili wa kuwazaa Lourdes Leon na Rocco Ritchie, pamoja pia na watoto wawili ambao aliwaadopt kutoka nchini humo, David Banda na Mercy James.
Hizi ni picha mbalimbali akiwa nchini Humo.
Hii ni wakati alipotembelea Shule ya Msingi Mikoko huko Malawi
Hata hivyo katika ziara hii, Madonna ameingia katika mgogoro na serikali ya Malawi baada ya taasisi yake ya misaada kupotosha ukweli kuhusu misaada anayotoa kwa sekta ya elimu nchini humo.
Waziri wa Elimu wa Malawi Eunice Kazembe amesema Madonna amejenga madarasa kwenye shule zilizopo na wala si shule nzima kama taasisi yake inavyodai.
Kauli hiyo ya serikali ya Malawi imetolewa wakati huu Madonna akitembelea shule 10 nchini humo ambazo taasisi yake ilidai zimejengwa na Madonna.
Credit Photos & Story: sammisago.com
