Mamia ya watu akiwemo Rais Googluck Jonathan wa Nigeria wamehudhuria mazishi ya mwandishi maarufu wa riwaya Chinua Achebe yaliyofanyika katika mji wa Ogidi kaskazini mwa Nigeria.
Viongozi wa serikali na wabunge walimsifu Achebe aliewapinga wanasiasa wala rushwa na mara mbili mwandishi huyo alikataa kupokea tuzo za heshima za kitaifa.
Hayati Achebe aliinukia kupata umaarufu kutokana na riwaya yake inayoitwa “mambo yanasambaratika” iliyochapishwa mnamo mwaka 1958.
Riwaya hiyo ni fumbo juu ya jinsi jamii ya jadi barani Afrika ilivyokuwa inasambaratika kutokana na ujio wa wakoloni na ilifanikiwa kuuza nakala milioni nane duniani kote.
Riwaya ya “mambo yanasambaratika” ilifasiriwa katika lugha 50.
Watu wa Nigeria wamemwita Chinua Achebe kuwa ni tai aliepo juu ya mti wa Iroko.