Washukiwa wawili wamekamatwa na polisi London kwa kumuua mwanajeshi
Mwanajeshi aliyeuawa katika kile kinachoshukiwa kuwa shambulizi la kigaidi mjini London, anatarajiwa kutajwa baadaye leo. Polisi wamewakamata washukiwa wawili na kuwazuilia hospitalini huku wakipokea matibabu.
Hata hivyo familia ya mwanajeshi huyo imefahamaishwa kuhusu kifo chake.
Muda mfupi baada ya mauaji kufanyika mtaa wa Woolwich, mwanaume mmoja aliyekuwa na damu mikononi mwake, alipigwa picha akisema kuwa alifanya shambulizi hilo kwa sababu wanajeshi wa Uuingereza huwaua waisilamu kila siku.
Wanaume wawili walipigwa risasi na polisi katika eneo la mauaji. Mmoja wao yuko katika hali mahututi.
Waziri mkuu David Cameron, alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa dharura uiliofanyika baada ya shambulizi hilo na kuahidi kutoa taarifa baadaye kuhusu tukio hilo.
Usalama umedhibitiwa katika kambi za jeshi kote mjini London, na wizara ya ulinzi imetoa maagizo kwao kuficha mavazi yao ya kijeshi.
Washukiwa wawili, walipigwa risasi na kujeruhiwa na polisi baada ya kufanya shambulizi lao.
Walioshuhudia tukio hilo walisema mwathiriwa alinyongwa na wanaume wawili waliokuwa wanasema ”Allahu Akbar (yaani Mungu ni Mkubwa ) kwa sauti ya juu
Wanaume hao hawakujaribu hata kidogo kutoroka na waliwataka walioshuhudia kitendo chao kuwapiga picha pamoja na mwanajeshi waliyemuua.
Katika kanda ya video iliyochezwa na shirika la habari la ITV, mmoja wa washukiwa alionekana akiwa amebeba kisu mkononi huku akitoa matamshi wa kisiasa.
“mnadhani wanasiasa watakufa? Aliuliza. “hapana, itakuwa kila mtu kama nyinyi na watoto wenu. Kwa hivyo waueni , waambieni warejeshe wanajeshi wetu ili muweze kuishi kwa amani,” aliongeza kusema mshukiwa huyo. Hata hivyo polisi walimpiga risasi na kumjeruhi