Mara kwa mara tumesikia ndoa za mastaa ambazo zimedumu kwa muda mfupi lakini itakuwa vizuri tukitaja ndoa za mastaa ambazo zimedumu kwa muda mrefu, unaweza ukasema ni za watu wa zamani yote kwa yote tunahitaji kuona ndoa ambazo ni mfano na watu hao kweli wamezitendea haki ndoa zao. Mastaa hawa wanadhihirsha kwamba sio mastaa wote ndoa zao zijadumu na familia ni ktu ambacho wamekuwa wakiipa kipaumbele…Na hawa ndo mastaa ambao ndo zao zimedumu:-
1. Rita Wilson and Tom Hanks Walioana mwaka 1988 ni hiyo ni karibu miaka 25 ni miongo miwili nanusu, wana watoto wawili Truman na Chester na Tom pia ana watoto wawili katika ndoa yake ya kwanza ambao ni Colin na Elizabeth.
2. Kurt Russel na Goldie Hawn mara ya kwanza walikutana Goldie akiwa na miaka 21 Kurt aakiwa na miaka 16 kabla ya kuungana mwaka 1983 ingawa haikuwa ndoa rasmi, wawili hawa wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 25 na bado penzi lao linachanua. Goldie ana binti anaitwa Kate Hudson na anamchukulia Kurt Russel kama baba yake, ingawa sio mtoto wake wa kumzaa Kurt amekuwa akimsaidia na wao pamoja wana mtoto anaitwa Wyatt ana miaka 26.
3. Matthew Broderick and Sarah Jessica Parker walioana mwaka 1997 na wana watoto watatu ndoa yao ikiwa na miaka 15, wakiwa ni mastaa akubwa katika filamu Hollywood
4. David and Victoria Beckham waliona mwaka 1999 na harusi yao ilihudhuriwa na watu 29 tu, Haijalishi kama wewe ni shabiki wao au laaah!! Kila wakati wameonekana wakifurahia ndoa yao na wameendelea kuwa na ndoa imara na mfano wa kuigwa.
5.David na Iman Bowie ni wapenzi wanaopendeza mwanamitindo na rock star, Rock star kutoka Uingereza na mwanamitindo kutoka Somalia walioana mwaka 1992 wana mtoto wa kike anaitwa Alexandria Zahra.
6.Kyra Sedgwick na Kevin Bacon walioana zaidi ya miaka 22 iliyopita, Kevin Bacon kuikweli ameunganishwa na mke wake alishaulizwa siri ya ndoa yao kudumu akasema “I think you have to got to keep fights clean and sex dirty”
7.Tim Mcgraw na Faith Hill wawili hawa walioana mwaka 1996 wana watoto 3.
8.Gavin Rossdale na Gwen Stefan wanamuziki wanaopendeza walioana mwaka 2002 na wana watoto wawili wakiume, katika mahojiano hivi karibuni Gwen alisema kuzaa na Gavin ni muunganisho mzuri hajapata kuona.
9. Sarah Michelle Prinze (Gellar) na Freddie Prinze Jr walioana mwaka 2002 ndoa yao imezidi kuwa imara siku baada ya siku, Freddie alikutana na Sarah kwenye set ya mwaka 1997 ya I know what you did last summer lakini hawakuanza mahusiano mpaka mwaka 2000 na Sarah alibadilisha jina lake la mwisho akajiita Prinze wakati ndoa yao ikitimiza miaka 5.
10. Catherine Zeta Jones na Michael Douglas walioana mwaka 2000 na katika mahojiano ya hivi karibuni Michael Douglas alisema ndoa inaendelea vizuri na kwamba Catherine ni mke mwema na anamsupport kwa kila kitu.
11. Bono na Ali Hewson, Bono anakubali kwamba kuolewa na mume wake haikuwa rahisi lakini wanakumbuka vitu vingi ambavyo vinafanya ndoa yao kuwa imara. Bono na Ali walioana mwaka 1982 na wana watoto wawili wa kike, Jordan na Memphis Eve na wawili wa kiume Elijah Bob Ptricious Guggi Q na John Abraham.
12.Denzel na Pauleta Washington walikutana kwenye set ya filamu ya “Wilma” Juni 25 1983, wana watoto wanne, wa kike anaitwa Katia, wa kiume anaitwa John David na mapacha Olivia na Malcolm. Pauleta na Denzel Washington harusi yao ilifungwa tena upya mwaka 1995 nchini Afrika ya kusini na Askofu Desmond Tutu, ingawa kulikuwa na uvumi kwa wawili hawa kuachana lakini wapo pamoja na wanaonekana wakiwa na furaha baada ya miaka mingi ya ndoa yao.
13. Mwaka 1980 Samuel L. Jackson alimuoa La Tanya Richardson ambae alikuwa ni muandaaji wa wa kipindi maarufu cha michezo na muigizaji machachari, walipata mtoto wao wa kwanza anaeitwa Zoe 1982 ambae ni anajitegemea katika filamu na mtayarushaji wa kipindi cha televisheni kwa sasa.
14. Ozzy na Sharon Osbourne ni kati ya wapenzi waliodumu sana katika Hollywood, Ozzy alikutana na Sharon akiwa na miaka 18, alimuoa Sharon mwaka 1982 Julai 4 na alifanya hivyo ili kila inapofika siku ya kusherekea siku ya kupata uhuru nay eye ndo anasherekea pia alifanya hivyo ili asisahau.Ingawa mwanzo mwa ndoa yao walishaachana kutokana na ulevi na madawa ya kulevya kwa Ozzy na ugomvi lakini wamekuwa ni watu ambao wamedumu sana katika Hollywood, wana watoto watatu Aimee, Kelly na Jack.
15. Danny Devito na Rhea Perlman
Ni kati ya ndoa zinazofurahisha na imedumu kwa muda mrefu katika Hollywood, walioana mwaka 1982 January 28 na wana mtoto wa kume anaitwa Jacob, na wawili wa kike Lucy na Grace. Mwaka 2012 mashabiki na watu wote katika tasnia ya burudani walishtushwa pale Danny na Rhea walipotangaza kuachana kwao baada ya miaka 30 ya ndoa kwa bahati nzuri waliweka mambo sawa na wanaendelea pamoja. Hawaamini uvumi na wanapendana sana na labda inawasiadia kuwa moja ya wapenzi waliodumu zaidi katika Hollywood.