Beyonce na Jay-Z wanadaiwa kuelekea kupeana talaka itakayogharimu dola bilioni 1. Kwa mujibu wa jarida la Marekani la wanandoa hao wanakabiliwa na talaka yenye gharama kubwa zaidi kuwahi kutokea kwa mastaa.
Inadaiwa kuwa Jay amekuwa akitembea na wanawake wengine. Jarida hilo limesema wapenzi hao wenye nguvu wamekuwa wakigombana mara kwa mara na wote wanaoneana wivu kupita kiasi. Chanzo kimoja kimesema Beyonce anaficha kutengana kwao kwa sasa.
Ripoti zinadai kuwa Bey na Jay hawana furaha kama wanavyoenekana hadharani. Beyonce ameifuta tattoo ya kwenye kidole chake cha pete ya ndoa kwakuwa uhusiano wao unafeli.