Msanii wa muziki wa kufoka foka Kutoka Tanzania Ney Wa Mitego anayetamba kwa sasa na Wimbo wake wa Muziki Gani, Huku Akiwa Ametoa Wimbo Mpya Kwa sasa unaoitwa NAKULA UJANA, Amesema leo alipotembelea office Za Magic Fm wakati wa Mahojiano na Katika Kipindi Cha Busati Kinachoongozwa na Mishi B, Allen Kassiga na Dj Muta kuwa anatarajia kutoa misaada kwenye vituo vinavyolela watoto Yatima hapa Dar Es Salaam na Moja Ya Mikoa Hapa Tanzania.
Kwa Maelezo ya Ney Ni Kwamba kwake hii ilikuwa kama nadhiri kabla hajapata mafanikio kuwa kama atafanikiwa japo kidogo basi aliahidi kwa mungu kuwa atasaidia wale wsionacho, hatimae ahadi lazima itekelezwe hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo watu mbali mbali wamekuwa wakitoa na kushare furaha zao pamoja na watu mbali mbali hasa wasiojiweza
watangazaji Wa Kipindi Cha Busati Magic FM Mish B, na Allen Peter Kasiga wakati wa mahojiano na Msanii Ney