
Kipi ni stories hapa kwa sababu hakuna mwanamke aliyeolewa anaweza kwenda kutafuta kitu bila maelekezo ya mpenzi wake, nani hapa anahusika ni Jay Z. Dunia imepasuka kwa uvumi kwamba Beyonce ameonekana akiangalia nyumba ya thamani ya dola 21.5, yenye eneo la mraba 4,054.
Embu fahamu hili, nyumba hiyo iko karibu na mjengo wa Katie Holmes aliokokwenda wakati akiachana na Tom Cruise, kitu ambacho kinaweza kikawa na maana fulani kwamba na Beyonce ndo anataka kwenda baada ya kuachana Jay Z.
Wakati huo huo wikiendi iliyoisha, chanzo kingine kiliongea na Page Six kikisema nguvu kutoka mbinguni tu ndo zitaweza kusaidia ndoa ya wawili hao hadi sasa haijalishi picha ngapi walizopiga wakionekana kama familia yenye furaha zikiwa zimepostiwa na Beyonce kwenye ukuraa wake wa instagram.
Pale mwanaume au mwanamke wako anapokuwa haridhishwi kutoka kwako, inaweza ikawa kihisia lakini sio lazima kimapenzi, huwa wanafanya vitu kimya kimya kilieleza chanzo kimoja.
Ugomvi wa kwenye lifti kati ya Solange na shemeji yake yani Jay Z ule ulikuwa ni ishara ya kwanza ya wazi ya mpasuko wa msingi wa ndoa yao, Page Six imeongeza kwamba ugomvui ule wikiendi ile ulisababishwa kwa sababu baada Met Gala ile Jay Z alikuwa anapanga akakutane na Rihanna……..Rihanna? Yes Rihanna…
Tour yao ya On the run inaisha katikati ya mwezi wa Septemba.
Kama Jay Z na Beyonce hawataachana basi itatakiwa watoe part 2 ya “Kipi sijasikia” ya Profesa Jay kwa sababu mambo kibao yameshasemwa kuhusiana na ndoa yao ikiwemo michepuko, ugomvi wa kifamilia na mengine.
