
Taarifa kutokana na Nairobi Wire, kundi la P.Unit linaweza likawa linaelekea kutengana baada ya memba mmoja wa kundi hilo kutangaza kama kuachana na muziki.
Maneno yaliyoenea mitaani ni kwamba mshikaji Bon Eye na Frasha wameteangaza wakati wa Industry night pale Galileo lounge wiki iliyopita.
Wawili hao ambao waliunda kundi la watu watatu kundi lililoleta ladha tofauti kwenye muziki wa genge, walitangaza kutengana na kila mmoja kufanya kazi kivyake kimuziki na biashara pia.
Ngoma yao ya mwisho waliyotoa wakiwa pamoja inaitwa L.O.V.E ngoma ambayo haikufanya poa sana na kundi linaweza likawa linakutana na wakati mgumu ambao hata makundi mengine yanakutana nao.
Kiukweli hii haitakuwa mara ya kwanza nchini Kenya, Kundi la Camp Mulla pia memba mmoja alitengana na wenzake kwenda kufanya muziki akiwa peke yake na Sauti Sol kumekuwa na uvumi kwamba kunataka kutokea kinachotokea kwenye makundi mengine lakini wamekuwa imara wajaruhusu hilo kutokea.
