
Mkali ambae inasemekana amepigana chini na mpenzi wake Safaree na mshikaji kufuta picha ya Nick Minaj na jina lake kwenye kifua, mkali huyo wa Anaconda anaona hakuna ishu ya kupoteza muda kwenye kitu hasi kwa sasa ametanganaza ngoma yake mpya inayoitwa “Only” akiwa na Lil Wayne, Drake na Chriss Brown.
Nicki Minaj amepata mafanikio katika maisha yake ya muziki na single ya “Anaconda” imeongeza mafanikio zaidi katika maisha yake ya muziki.
The mammoth ni ngoma ya pili kutoka albamu ya mwanadada huyo inayokuja inayoitwa The Pink Print ambayo imefikia namba 2 kwenye Billlboard Hot 100, kwa sasa Nicki hapotezi muda wowote kufuatia mafanikio ya wimbo na video na ngoma ya tatu.
Kutokana na cover art ambayo imetolewa kupitia instagram page ya Nicki, repa huyo kutoka Young Money yuko na wakali kutoka kwenye lebo yake na muimbaji bora duniani Chriss Brown ambao ndio wanafanya ngoma ya “Only”. Drake na Lil Wayne wote wawili wameapnagwa kutokea kwenye ngoma hiyo ambayo imepangwa kutoka Jumanne 28 siku ya kesho.
Wasanii walioshirikishwa kwenye “Only” pia walitokea kwenye albamu yam kali huyo ya Roman Reloaded.
Tangazo la wimbo huo mpya unavunja uvumi uliokuwa umeenea kwamba Drake hatokuwepo kwenye albamu hiyo ya tatu Nicki Minaj, albamu imepangwa kutoka Novemba 24.
