
Ni Katika muendelezo wa kampeni ya jishindie Nokia Asha na Daladala Beats,leo amepatikana mshindi wa pili,baada ya zawadi ya kwanza kunyakuliwa na Flavian Gamba kutoka Kiwalani Dar es Salaam wiki iliyopita
Wiki hii mwana dada Nurat Nyupe kutoka Msasani Dar es Salaam ameweza kujishindia simu ya mkononi aina ya Nokia Asha pamoja na t-shirt ya Nokia na kofia.
Pichani ni Meneja wa Magic FM Dativus Mango akikabidhi zawadi hizo.
Kwa upande wake Nurat amefurahi sana kwa kuweza kuibuka mshindi na kuwasihi wasikilizaji wengine wa Daladala Beat kuendelea kusikiliza na kujaribu bahati yao kwa kushiriki kujibu maswali mepesi tu yanayohusiana na Nokia na kipindi cha Daladala Beat kinachoanza saa 7mchana mpaka saa 10jioni kupitia Magic Fm jumatatu hadi Ijumaa.
