Msanii mkubwa Afrika Oliver Rudaviro Mtukudzi amepewa heshima ya Dokta kutoka kwa kutangaza sanaa ya Zimbabwe na utu wake kwa jamii ya Zimbabwe na kutangaza amani pamoja kupigania maenedlep utu nchini huko.
Mtukuzi pia ameongoza vizuri sanaa kwa ujumla ya Zimbabwe bila kupoteza uhalisia wake.
Jina lingine wanalomuita huko Zimbabwe ni Tuku, Oliver Mtukuzi amekuwa mstari wa mbele katika kupigania amani na maendeleo huku akiwa na UN katika kampeni mbalimbali za maendeleo Afrika na wimbo wake wa Ngoromera (Hatidi Hondo) kutoka katika albamu yake inayoitwa Bvuma – Tolerence yani Uvumilivu na kuonyesha jinsi alivyojitoa katika kupigani amani.
Kweli Oliver Mtukuzi anastahili kupewa heshima hiyo ya Dokta kwani amekuwa mstari wa mbele katika kutaka watu wapendane na kuacha mambo ambayo yanaweza kuwafanya waingie katika vita na kupoteza amani. Hii ni barua ambayo aliandikwa Oliver Mtukuzi na kuibali ilisomeka hivi:
“The International Institute of Philosophy, though its Zimbabwe Office and in consultation with the Philanthropy Institute of Zimbabwe, incorporating the African Institute of Philanthropy (AIP) and the Women’s Institute of Philanthropy (WIP), is humbled and honoured to advise that you Mr Oliver Mtukudzi will, should you accept this highly esteemed Honorary Doctorate Degree of Humane Letters, (you will) be officially addressed as Dr. Oliver Mtukudzi, Doctor of Humane Letters, DHL.”