
Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis wa Kwanza ametawazwa Rasmi kuliongoza kanisa hilo katika ibada iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro Mjini Vatican.
Maelfu ya watu kutoka nchi mbali mbali duniani wamekusanyika Vatican kushuhudia kuidhinishwa Rasmi kwa kiongozi huyo mpya wa kanisa wakiwemo viongozi wa kidini na kisiasa ambapo katika mahubiri yake amesisitiza kuleta mabadikiko makubwa.
Papa Francis wa kwanza alichaguliwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya Papa Benedicto wa kumi na sita aliyejiuzulu mwishoni mwa mwezi wa pili kwa sababu ya Umri wake mkubwa pamoja na hali yake ya kiafya
