Maza akiwa Mgeni Rasmi wa shughuli yake Mama Asha Bilali
Jana Maza kupitia kampuni yake ya Maznat Bridal iliandaa sherehe za kuazimisha miaka kumi ya huduma zake kwa jamii, Maznat ni kampuni inayojihusisha na maswala ya kupamba maharusi kushona nguo za maharusi na sherehe mbali mbali na swala zima la huduma za urembo kwa akina mama (beauty clinic)
Sherehe hizo zilihudhuriwa na wanawake mbalimbali katika nyazifa tofauti huku mgeni Rasmi akiwa ni mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal
sherehe hiyo ilinogeshwa na biurudani toka kwa THT dancers na Mzee Yusuph wa Jahazi
Zaidi ya kuadhimisha miaka kumi ya mafanikio katika huduma yake hiyo kwa jamii lakini pia kampuni hiyo ilizindua shule ya mambo ya urembo na kituo cha kulelea watoto yatima.
Zaidi ya kwamba Maza ni mwanamke msomi wa musters ya Sheria hakuwa tayari kuajiriwa bali alisoma kwa ajili ya kutengeneza ajira kwa wengine ndoto alioitimiza kwa kuamua kiufanya kitu anachokipenda na kuhifadhi elimu yake kwa akiba ya baadaye huku akifanikiwa zaidi kutokana na elimu alioipata.
ujumbe wa siku hiyo ulikua ‘IF YOU DREAM IT, YOU CAN DO IT’ TUNAWEZA.
Angalia baadhi ya picha za tukio hilo:
Maza Akiwa na wageni wake katika meza kuu
kulikua na tukio la keki katika kuashiria kutimiza miaka kumi, cake iliokatwa na Mgeni rasmi wa tukio hilo Mama Asha Bilal na Maza
huu ulikua ni uzinduzi wa shule mpya ya mambo ya urembo itakayokuwa chini ya Maznat Bridal
kulikua na tukio la ufunguaji wa Champaign kazi iliofanywa na kina kaka kumu waliovalia sare ikiwa ni ishara ya miaka kumi
hapa ndipo mzee Yusuf alipo wachezesha Kina mama mduariko
mama wa salmamsangi.com ndani, kaenda na theme kama kawaida
Maza akisema lolote mbele ya wageni waalikwa
picha zaidi zaja Red carpet na nyinginezo usibonyeze kidude