
Kampuni ya urushaji matangazo ya kimataifa ya DSTV jana imesherekea sherehe za kufunga mwaka ambapo imewezakujumuika na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa kampuni hiyo katika kuufunga mwaka 2013.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo jijini dar es salaam meneja uhusiano wa Dstv bi. Barbara Kambogi amesema
kumekuwepo na mafanikio makubwa katika msimu wa mwaka huu na hasa katika shindano la big brother ambalo lilifanyika
katika msimu huu na kuonekana tanzania kushiriki vema katika shindano hilo.
Aidha bi.Kambogi amesema hivi karibuni DSTV ilichezesha mashindano ya uchoraji pamoja na uandikaji wa insha kwa
wanafunzi wa shule za sekondari ambapoa washindi walipatikana na walikabidhiwa zawadi jana katika hafla hiyo.
Shule zilizofanya vizuri katika shindano hilo ni pamoja na shule ya sekondari mzumbe na shule ya sekondari Aghakhani
mzizima ya jijini dar es salaam.
meneja uhusiano wa Dstv bi. Barbara Kambogi Akiongea na wageni waalikwa

Resty Ngonyani meneja masoko wa Channel Ten Akiwa na Meneja huduma maendelea ya wafanyakazi wa channel ten Sakia
