Lady Jay Dee akiwa Mahakamani ili kusimama kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo kesho mei 27 .Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.
LADY JAY DEE AKIWA NA MUME WAKE GADNER HABASH
“Hili ndilo shtaka lenyewe kwa hivyo sisi hatuwezi kusema chochote kwa sasa tunaelekea kwa mwanasheria wetu ili kuanza kuishughulikia kesi hii,” alisema Gadna Habash mume wa mwanamuziki huyo.
Kabla ya kufika mahakamani hapo mchana, mwanamuziki huyo alitoa mada katika jukwaa la sanaa Basata ambako alizungumzia changamoto nyingi zilizopo katika kufikia mafanikio kwenye sekta ya muziki.
Wakati kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Mei 27, siku nne baadaye Jaydee anasherehekea miaka yake 13 tangu aingie rasmi katika sekta ya muziki ambapoa sherehe hizo zitafanyika Nyumbani Lounge tarehe 31 mwezi may mwaka 2013 kwa kiingilio cha shs ELFU ISHIRINI NA SEAT MAALUM ELFU KHAMSINI.