Hivi karibuni kupitia mtandao wake wa Face Book Mwanamuziki mkubwa Tanzania mwanadada Lady Jay Dee ametupia picha alizopiga na mwanamuziki Mashuhuri na mkongwe Afrika na Dunia Self Keita kutoka mali
Lady Jay Dee aliandika ya kwamaba amekutana na mwanamuziki huyo huko Nairobi Nchini Kenya katika Hotel Ya Southern Sun wakati wa kupata kifungua kinywa ambapo alijikuta akitetemeka mpaka kutaka kudondosha sahani yake
Hata hivyo aliongeza kwa kuandika “leo nimekaa na Self Keita, Tumeshake Hands, Tume Hug, tumepiga mapicha na mbali ya yote kuna kitu kikubwa kinakuja kati yangu na yake”
Kwa kawaida ya lady Jay Dee huwa hafanyagi makosa mara anapopata nafasi ya kukutana na wasanii wakubwa kama hawa hivyo tutarajie Jambo baada ya hapa
Lady Jay dee ameshawahi kufanya kolabo na msanii mwengine mkubwa sana katika bara la Afrika na Dunia kutoka Zimbabwe Oliver Mtukuzi wimbo unaitwa MiMI.
Tazama picha hapa lady Jay Dee akiwa katika pozz tofauti tofauti na Mwanamuziki Self Keita