
Hatimae jana jumapili kampuni ya Nsiima inayoshughulika na maswala ya Catering yenye makao yake makuu mjini Morogoro iliadhimisha Siku yao waliyoipa jina la Nsiima Day ambapo pamoja na mambo mengine walitoa misaada katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu pia kulikua na michezo mbali mbali kama utakavyoona katika picha wafanyakazi wa kampuni waloishiriki pia katika chakula cha pamoja nyama choma na kucheza mziki pamoja

Mkurugenzi Mtendaji wa Nsiima Catering Services Mama Immaculata Rutatora akiwa ameshika watoto waliotembelewa katika kituo cha kuwalelea

Mkurugenzi Mtendaji wa Nsiima Catering Services Mama Immaculata Rutatora Aliyevaa kofia akiongozana na wafanyakazi wa kampuni hiyo leo asubuhi Walipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole Mjini Morogoro

Wafanyakazi wa Nsiima Catering Services Wakiwa wamebeba vitu mbalimbalia kwa ajili ya kituo cha watoto yatima Cha Mgolole Mkoani Morogoro

Meneja masoko wa kampuni ya Nsiima Jackline Rutatora Aliyevaa Kofia akiwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo
