
Mama mzazi wa Msanii Profesa Jay amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kugongwa na gari maeneo ya mbezi juu jijini Dar alikokuwa anaishi na mwanae.
Bi. Rosemary Manjara Haule aligongwa na gari akiwa anavuka barabara kuelekea dukani mida ya saa mbili na kwamba baada ya kugongwa wasamaria wema walimkimbiza hospitali ya Tumbi kwa kutumia bajaji ambako mauti ilimkuta huko
Profesa Jay amethibitisha hilo na kudai kwamba ilikuwa ni vigumu sana kuamini.
Profesa anasema kwamba wakati anapigiwa simu alikuwa katika mgahawa wa nyumbani lounge,Namanga Dar ambako alikuwa katika kikao na Lady jaydee na mumewe.
“MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NAGARI….NJONI KOPOLISINAANDIKISHA…. MWANANGU NAKUFA…. ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI…” ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
