Popozzzzzz wamponza Mwanasoka Samuel Eto’o
Mara hii ni katika duka la saa za bei ghali sana, ambapo mwanasoka huyo aliyewahi kuwa mshindi wa kikombe cha mchezaji bora wa mpira Africa huko nyuma Alisema Akiwa na ndugu yake ilikuwa March 12 aliingia katika Duka La saa za bei ghali ili anunue saa katika duka moja linalouza saa hizo lakini wahudumu wa duka hilo waligoma kumuuzia kwasababu kuna Mnigeria alitumia credit card Fake siku za nyuma katoka duka hilo
Eto’o ambaye anamiliki kiasi cha $100million alisema aliingia katika duka na ndugu yake kununua saa yenye thamani ya£10,000 lakini muuza duka aliwaangalia kwa woga na na kuwaacha watizame saa waliokuwa wanahitaji
“Nilikwenda kununua saa katika duka ambalo halipo mbali na nyumba yangu, saa niliyotaka kuiona ilikuwa ghali kiasi,nilimuuliza muuzaji ambaye nae ni mweusi, unaweza kunionyesha hii saa tafadhali? kwanza nikamuona amegeuka na kumtazama muuza duka mwenzie kama akashangaa na kujiuliza mmh nifanyeje hapa?
Hata Hivyo Akaniacha Nitazame tena saa, nikatazama na kusema sawa nitanunua nikampa credit Card yangu na alipoipeleka kwenye machine akarudi akasema haitumiki”
Eto’o, ambaye ni mwanasoka tajiri katika nafasi ya saba duniani alisema.
Eto’o aliongeza kuwa kumuuliza “imekataa au hukutaka ikubalike?’ alimuuliza muuza duka
Aliliambia shirika la habari la CNN
“Ndugu yangu alimuuliza ‘Nini kinaendelea? akajibu, Hakuna,hakuna . Lakini Akasema, ‘Hapana kwasababu wakati tunaingia niliona jinsi gani mlivyotutazama, Kaka yangu ana uwezo wa kununua saa hii lakini kwa jinsi mlivyomuhudumia ni kwasababu yeye ni mweusi na mnadhani hawezi kumudu kununua saa hii
“Mwanamke huyo akaamua kujieleza ndipo alipofunguka na kusema : Hapana Ni kwasababu tu tulipata mteja wa kinaijeria ambaye alikuja na credit Card Fake, Huwezi amini nilivyojisikia kwasababu niliona kweli kama mtu mmoja akifanya kosa basi wote wanaonekana wakosaji sidhani kama alifanya ubaguzi lakini kudhani tu kuwa watu wote weusi wana tabia moja”