![](http://salmamsangi.com/wp-content/uploads/2015/11/ugly-160x100.jpg)
Siku ya jana imeripotiwa mkali Future na Ciara wameachana na sio wanandoa tena na imeripotiwa kwamba Future yeye ndiye alietaka waachane na Ciara.
Future alimshangaza Ciara na pete ya 15 carat diamond wikiendi taarifa za Associate Press kupitia abcnews.go.com zilieleza.
Story hiyo iliripotiwa imethibitishwa msemaji wao Chris Chamber, wawili hao ndoa yao ilikuwa ya kimahakama kwa muda wa mwaka mmoja hakukuwa na tarehe ya harusi. Future na Ciara wameachana wakati Ciara alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa na baadae akatweet “Today Has 2 Be Like One Of The Sweetest Days Of My Life! #TheBestBirthdayEver YOEYOEYOE”
Future ameshirikiana kimuziki na wasanii wakali akiwemo Miley Cyrus, Rihanna na mpenzi wake mwenyewe, kwa sasa repa huyo ambae pia ni producer yuko kwenye tour ya Drake ya “Would you like a tour? “ Future na Drake ilisharipotiwa walizenguana lakini wakamalizana kabla ya tour kuanza.
Kwa sasa Ciara anatengeneza ngoma nyingine mpya, Alabamu ya Ciara ya kwanza Goodies ilifika Platinum mara 3 na ilimfanya Ciara kushinda tuzo ya Grammy mwaka 2005. Pia aliingia top 10 ya Billboard, Ciara ameshafanya ngoma na wakali kama Justin Timberlake, Bow Wow, Miss Eliott na mpenzi wake walioachana Future.
Kikubwa kilichovunja ndoa hii inasemekana ni kwa Future kutokuwa mwaminifu katika ndoa ndicho kilichosababisha kuachana, Wawili hao wana mtoto mmoja wa kiume, na toka Ciara ajifungue inaripotiwa hawakuwahi kuonekana pamoja tena mpaka inaripotiwa kuachana, Future peke yake ndo alikuwa akitoka mwenyewe sehemu sehemu za kuparty.
![Top 20 Bongoflava](http://salmamsangi.com/wp-content/uploads/2013/10/Unbenannt.jpg)