
Ni kawaida kwa Prezzo kuchanwa na wapenzi wake mara nyingi, wapenzi anaokuwa nao mwisho wake huwa mbaya.
Mara nyingi tumeona kupitia TV na blogs kuhusu mahusiano ya Prezzo kwa wakati yakiwa yanachanua.
Mfano Chagga Barbie mwanadada wa kichaga mzuuri kutoka Tanzania nae walichanana sana hadi mambo ya ndani, ikaja kwa Huddah Monroe wote hawa waliweka mambo ya ndani hadharani kuchanana sana mpaka unafunga mdomo kwa aibu.
Mabinti hawa wamekuwa wakisema Prezzo ni muongo wala hana hela anadanganya tu anasema ni tajiri wakati ni masiki tu.
Mtu mwingine anaweza akakataa haya yaliyosemwa na wakina dada hawa kwa sababu ikaonekana ni chuki tu baada ya kuachana.
Ameibuka mwanamke wake ambae wameachana nae anayeitwa Daisy Kiplagat amekuja nae ameanza kumchana Prezzo akiwa ni watatu baada ya Chaga Barbie na Huddah.
Daisy amesema kupitia face book baada ya kuandika kwa urefu kuhusu mahusiano yake na Prezzo, wamezaa mtoto mmoja, Daisy anasema Prezzo hawezi hata kumlipia ada mtoto wao mpaka anaenda kukopa kwa rafiki yake na anaenda kulipa ada.
Anasema Prezzo anaonekana kwenye vyombo vya habari akijisifia kuwa anapesa lakini hakuna kitu ni muongo.
Hata hampi pesa za kumsaidia mtoto wake ndo maaana alienda mahakamani akidai pesa za kumsaidia mtoto.
Baada ya malalamiko hayo Prezzo amepigiwa simu aseme ili tujue upande wa pili wa stories ili lakini hakupatikana, lakini siku zijazo kupitia Dabo Dabo Time tutajua mpango mzima.
