David Kibuuka wa kampuni ya One Nation Entertainment ya Uganda, alikuwa akihusika kuandaa tamasha la Chris Martin, lakini tamasha hilo likawa ni matatizo na ilipewa nyota 5 katika show zilizofeli nchini Uganda. Kama hilo halitoshi, Polisi wa uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebe walikuwa wakimtafuta promota huyo David Kibuuka kwa kuwa na deni kubwa.
Wakati huo huo tayari ameshakamatwa kwa kosa lingine.
Taarifa zimeenea kwamba amewekwa jela kwa kubook Aero beach na kuhairisha show, Aero beach inadai milioni 5 kwa hasara ambayo imepata kwa sababu ilikataa bookings za matamasha mengine kwa sababu David alikuwa amebook.