RAIA 360 kutoka China ambao wanafanya kazi katika kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara, hawana vibali vya kufanyia kazi hapa nchini.
Afisa Uhamiaji mkoa wa Mtwara Zakayo Mchele, amesema maafisa wake walitembelea kiwanda cha Dangote kuhakiki wafanyakazi kama wana vibali vya kufanya kazi nchini lakini walipofika kiwandani hapo hawakupata ushirikiano kutoka kwa Meneja wa kiwanda hicho.
Afisa Uhamiaji huyo amesema wageni wote wamekamatwa na idara ya uhamiaji na ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kuwafichua wageni ambao wanaendelea kuishi nchini bila kibali.