Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakisindikiwa na Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova baada ya kutembelea eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa mkuu wa polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova pamoja kushoto ni Mkuu wa mkowa wa Dar Es Salaam Sadiq mek Sadik
Picha: Ikulu
Maandishi :Mo blog
1 Comment
Hakuna lolote lile wizi mtupu,tuzo za kupendeleana tu