Taarifa za United Nations Development Programme, zinaonyesha robo tatu ya nchi zenye watu milioni 24, wanaishi chini ya mstari wa umasikini yani kwa maneno mengine ni masikini na karibu 70% wanaishi chini ya dola 2 kwa siku.
Lakini rais Jose Eduardo Dos Santos hakuona tatizo lolote kumualika msanii wa Hip Hop kutoka Marekani aende akaimbe kwenye party yake binafsi ya Christmas kwa kumlipa kiasi cha dola milioni 2.
Ingawa alipigiwa simu kutoka kwa Wanaharakati wa haki za binadamu na kumtaka aache kufanya concert kutokana na umasikini wa taifa hilo, Nicki Minaji alitia masikio pamba na alidondoka Angola na ndege binafsi kwa ajili ya show hiyo ambayo ilifanyika Jumamosi huko Luanda nchini Angola.
Dos Santos 73 kila wakati amekuwa akihusishwa na rushwa,matumizi mabaya ya pesa na tishio kwamba nchi hiyo inatajwa kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika, lakini watu wake wanaishi kwenye dimbwi la umasikini.