CEO wa zamani wa Death Row Records Suge Knight ametoka hospitali asubuhi jana, baada ya kutibiwa majeraha ya risasi alizopigwa Agosti 24 katika Pre Party ya MTV VMA.
Taarifa za TMZ zimeeleza kwamba Boss huyo wa zamani wa Death Row Records ametoka hospitali jana Agosti 27 pale katika hospitali ya Cedars-Sinai moda ya saa 12 asubuhi.
Taarifa zaidi zinasema kwamba Suge hatahitaji rehab ili kumsaidia kuponya majerah yake na ataweza kurudi nyumbani, ila anahitaji ufuatiliwaji wa karibu ili kujua maendeleo yake.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Suge Knight hatarajii kushirikiana na polisi katika uchunguzi wa tukio hilo lililosababisha apigwe risasi, video ya tukio hilo imetolewa lakini hakuna mtu aliyeweza kumtambua mtu alaiyefanya kitendo kile.
Suge Knight alipigwa mara sita mida ya mapema asubuhi Agosti 24 katika club ya usiku inayofahamika kama 1.OAK huko magharibi wa Hollywood California, kufuatia tukio hilo alipelekwa hospitali amabapo alifanyiwa upasuaji kutokana na majeraha aliyekuwa ameyapata. Baada ya kupigwa risasi hakuweza kutembea kutoka ndani ya club.
Suge Knight alikuwa akijulikana zaidi kwa kazi zake na Tupac kama mwanzilishi wa Death Row Records, mwaka 2006 Knight aliripotiwa kufilisika na mwaka 2008 Death Row Records iliuzwa.