J.Luchiano aliacha mixtape yake kwenye mlango wa kuingia kwa Rick Ross, Rapper huyo kutoka Atlanta alikamatwa wiki iliyopita kwa kukatiza kwenye nyumba ya Rick Ross,TMZ iliripoti.
Luchiano anasema aliacha mixtape yake kwa rapper huyo wa Miami kwenye mlango wake wa kuingilia ndani miezi miwili iliyopita,alipigiwa simu na mwanasheria wa Rozay, akimtaka afike ofisini kwake, anasema aliingizwa kwen5e mtego kwa sababu polisi walifika hapo na kumkamata kwa kosa hilo la kukatiza kwenye nyumba ya Rick Ross.
Mamlaka zinasema kwamba Luchiano aliruka fence ili kufikia nyumba ya Rick Ross na alipost picha kwenye mtandao akionekana akiwa kwenye nyumba hiyo, anasema alitumia njia ya pembeni kuingia lakini hakuruka ukuta.
Luchiano alitoka dhamana ya kiasi cha dola 3,500, Walinzi wa Rick Ross wanasema Rozay hakuhusika kwenye ishu hiyo ambayo imemuweka pabaya Luchiani.