
Boss wa kundi la MMG Rick Ross anafunguka nini atafanya kwake ili kuleta amani kati yake na mshindani wake wa siku nyingi 50 Cent. Beef ya Rick Ross na 50 Cent imegonga tena vichwa vya habari baada ya wakali hao kupeana maneno makali kupiti instagram wiki iliyopita.
Akiwa ameonekana kwenye show ya The Nightly Show With Larry Wilmore, Rick Ross anaulizwa kama atamaliza ubaguzi kama ishu ni kuwa marafiki na mshindani wake wa siku nyingi.
“Inatakiwa upende kwenda kutembea pamoja,mnatakiwa muende mle pamoja,muende sehemu mbali mbali pamoja,chochote,nyie ni marafiki, Je mtafanya hivyo? Anafunguka Larry Wilmore.
“Naacha ubaguzi,ambao mashabiki wanaridhia,nitamchukua mpaka Wing Stop tupate pepper wings ya limao,hicho ndicho nitakachokifanya” alijibu Rozay.
Daah! Hawa jamaa wakipatana itakuwa kitu kingine kikubwa sana kutokea katika Hip Hop world, watu wengi wanasubiri waone jamaa wakipatana na kufanya ngoma moja na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja.
