
Baada ya mkali Meek Mill kuendelea kuwa jela mpaka mwezi Oktoba kama ilivyotangazwa, na albamu yake ya Dreams Worth More Than Money kuharishwa kutoka Septemba 9 kama ilivyokuwa imepangwa, Boss wake mtu mzima Rozay ameona maisha lazima yaendelee wakati wakimsubiri Meek Mill kutoka jela.
Rapper Rick Ross ametangaza ujio wa album yake mpya na ya sita. Kwa mujibu wa Chanzo cha info hizi ni kwamba Rapper Rozay ametangaza tarehe 15 September 2014 kuwa album yake itaitwa Hood Billionaire na ndio inayofuata album yake ya Mastermind iliyotoka March 2014.
Septemba 14 mkali Rozay alitweet na kuandika #HoodBillionaire 1st Single.
Albamu ya kwanza ya Rick Ross inaitwa Port of Miami, ikafuatia na Trilla, ikaja Deeper than rap, the Teflon Don, albamu nyingine iliyokick sana ni God forgives, I don’t na ya mwisho iliyotoka March 3 mwaka huu ilikuwa ni Mastermind.
Tusubiri albamu yam kali Rozay ambayo tayri jina linajulikana ingawa hajatangaza lini inatoka….stay tune for the MMG Boss next albamu.
