Madaktari wa Bobbi Kristina Brown, mtoto wa Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, wameamua kumtoa kutoka katika hali ya coma, watu wameripoti Jumatano hii.
Bobbi Kristina alikimbizwa hospitali baada ya kukutwa ameanguka uso ukiwa umezama kwenye jakuzi hakiwa hajijui Januari 31.
Ataendelea kutumia mashine ikiwemo zinazotumika kumlisha kwa kipindi hiki watu waliongeza.
Chanzo kimoja cha karibu na familia kililiambia magazeti kwamba familia ya Bobbi wanatumaini na wanaomba atoke katika hali ya kutojifahamu, hapo ndipo itakapojulikana na kutoa majibu kama hali yake bado ni mbaya sana au laa kiliongeza chanzo hicho.
Mapema mwezi huu anayefanya kipindi cha televisheni cha “The Doctors” Rachael Ross alisema madakatari wamemuacha kwenye coma ili ubongo wake uendelee kupata nafuu.
“Kama ubongo haufanyi kazi, tunachoweza kufanya ni kufanya uwezekano ubongo wake usipate uvimbe zaidi na tunaweza kumpa muda zaidi ili ujitibu” alisema Ross
Kumtoa Bobbi katika coma itawaruhusu madakatari kujua kama hali ya Bobbi Kristina imeimarika kabisa na kuweza kufanya kitu chochote yeye mwenyewe.
Wakati madaktari wa Bobbi na familia wakitarajia majibu, mambo yasiyo ya kawaida yamekuwa yakiendelea nje, boyfriend wake anayeitwa Nick Gordon amekuwa na ugomvi na baba yake Bobbi Kristina kwenye twitter, akisema baba yake Bobbi Kristina Bobby Brown amemzuia kwenda hospitali kumtembelea Bobbi, imeripotiwa kwamba Gordon amefungua shauri akigomea polisi wa Georgia kwenda kusachi video iliyochukuliwa na kamera ulinzi.