Mkali wa Blurred line anajiribu kumrudisha mke wake Paula Patton, Alionyesha wazi kabisa Jumatatu wakati Tour yake ya ikiendelea ya Mea Culpa Tour na pia ameachia video ya wimbo unaitwa “Get Here Back” na akama kulikuwa na maswali yeyote yale kuhusu ngoma hiyo basi zimeonekana clips mtu ambae amewekwa amefanana na mke wake Paula Patton.
Katika video hiyo anaonekana anaimba mistari ambayo anajutia kilichotokea kwake na muigizaji huyo na katika video hiyo hiyo inaonekana mwanamke ambae anamuimbia aliyefanana na Patton mwishoni anakubali. Na kama kuna mtu anabisha kuhusu hilo kamera ilizoom nakuonyesha pete ya ndoa ya Robin.
Na katika video hiyo imeambatana na maneno ambayo yanaandikwa kwenye video wakati ikiendelea kama “ Naweza kuongea na wewe? Umeharibu kila kitu” Unakunywa sana, “Unaniudhi, Na siwezi kufanya mapenzi na wewe tena na kitu kingine kikubwa kilichoandikwa kwenye video hiyo aliandika “Nimeandika albamu yote kuhusu wewe” ambayo inafutiwa na neno “Sijali”
Kweli Robin Thicke ameamua kuonyesha mapenzi yake kwa mke wake Paula Patton ambae kwa sasa mambo sio fresh penzi lao linayumba lakini Robin anajaribu kulirudisha.