
Rick Ross alikosolewa sana baada ya kutishia kumuua mgombea urais nchini Marekani Donald Trump kwenye ngoma ya “Free Enterprise” ngoma inayoptaikana kwenye albamu ya “Black Market”, kulikuwa na ripoti kwambamaduka yaw al-Mart yaliiondoa albamu hiyo kutokana na mashairi hayo.
Akifanya mahojiano hivi karibuni na Rolling Stone, Rick Ross anaeleza maana ya mashahiri hayo “Assassinate Trump like I’m Zimmerman / Now accept these words as they came from Eminem.”
“Sitatea uhalifu juu ya Donald Trump au mtu yeyote, ni mauaji ya mashahiri” anasema Rapper huyo kutoka Miami. Huko ni kuwa mwanamashahiri, unayaweka maneno katika hali ya kisanaa, hakuna hali ya kihalifu kabisa kwenye moyo, nadhihirisha, ukweli ni kwamba, camera man wangu alikuwa msaidizi wa Trump (Caddy) kwenye uwanja wake wa golf kwa miaka 5 na anasema Trump yuko poa kuliko unavyodahania”
Aliulizwa kama Eminem amejiweka mbali kabisa na mashahiri yaliyojawa na mistari ya kihalifu kuliko marappers wengine kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.
“Nadhani hiyo ni sababu kubwa, ndo maana nilichachana huo mstari, labda hili swali lingeibuka lakini kiukweli sipo kwa ubaguzi wa mweusi au mweupe, marafiki wangu wengine wazuri ni weupe” alisema Rozay.
