Inaonekana kama hakuna utulivu katika himaya ya rapper Kanye West na mke wake mwanamitindo Kim Kardshian, wiki sita baada ya kupata mtoto wao wa pili anayeitwa Saint.
Kweli tuna tumaini hii sio kitu zaidi ya uvumi,
Kutokana na taaarifa mpya, kumuhusu couple inayotazamwa na watu wengi sana duniani wamekuwa wakibishana juu ya maisha yao ya baadae, Kanye West yeye anataka kuongeza familia na kupata mtoto wa tatu lakini Kim Kardashian alishaamua hapana.
“Lakini Kim anashikilia jambo hilo hilo kwamba Saint ndo alikuwa mtoto wake wa mwisho”
Madaktari wazi kabisa walisema kwamba kama Kim atapata mimba tena atajiweka yeye hatarini pamoja na mtoto aliyebeba mimba yake, Kim amezingatia hilo lakini inaonekana Kim hilo halimuingii akilini hata kidogo.
Kim Kardshian ana matatizo ya kiafya hasa pindi anapokuwa mjamzito, alipata matatizo hayo mara zote ya mimba zake mbili, na hadhani kama ataweza kubeba mimba ya tatu.
Chanzo kimoja kilieleza: “Kanye anadhani kwamba Kim asiwe na maamuzi hayo ya kudumu kwa ajili ya wakati ujao kwa sasa kwa sababu inasabbishwa na mwili wake”
Chanzo cha habari hii kutoka ndani ya familia ya Kanye kiliiambia Radar Online: “ Kanye anataka kuongeza familia lakini Kim amekamatia msimamo wake na anataka kufunga kizazi au IUD”