Hizi Ndio Sababu Tano ambazo zinatoa msisimko na kufanya usikose Kombe la dunia 2014 nchini Brazil, sababu ya kwanza kabisa ni timu ya Brazil na mashindano yanafanyika nyumbani kwake yeye ndo mwenyeji mbele ya mashabiki wake atakubali kuachia ubingwa?
Sababu ya pili ambayo inasabbaisha usikose kombe la dunia 2014 ni bingwa mtetezi kucharazwa na kuanza kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa baada ya kukubali kipigo cha magoli 4 – 1 kutoka kwa Uholanzi ambae alimuwekea kinyongo baada ya kufungwa katika fainali nchini Afrika kusini 2010.
Sababu ya tatu ni Uingereza kuvurugwa kabisa na mabingwa mara nne baada ya kufungwa na Italia 2 – 1, Je Uingereza atafanyaje mechi ijayo? Anakutana na Uruguay. Sababu ni timu iliyokuwa bora duniani na ghafla kushuka katika viwango vya soka duniani nia Ufaransa. Je kombe la dunia 2014 Brazil itarudisha heshima yake kama ile ya mwaka 1998.
Na sababu ya tano ni kwa wachezaji wawili wanaotawala soka la Ulaya na dunia na kuwa na rekodi nzuri katika vilabu vyao na kunyakua mataji mbalimbali lakini kwa bahati mbaya wote hawana rekodi nzuri katika kombe la dunia ni “Lionel Messi” na “Cristiano Ronaldo” Je wachezaji hawa watafanya yao na kupata mataji mbalimbali kama mchezaji bora, mfungaji bora na mengineyo? Tuendelee kucheck Kombe la dunia hizi zikiwa ni sababu tano zinazotufanya tusiache kuangalia Brazilika 2014.