
Rais Jakaya Kikwete amewapa pole na serikali imeanza kuuchukua hatua ikiwemo kutoa misaada ya kibinadamu kama chakula na ujenzi wa daraja..
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema hayo baada ya kutembelea eneo lililokumbwa na athari za mafuriko ikiwemo daraja la Magole linalokatiza mto Mkundi lililobomolewa na maji na kuonana na wananchi wa kijiji cha magole ambao Idadi ya kaya 2000 zimezingirwa na maji na amesema
Serikali imeahidi kuhakikisha ujenzi wa daraja la Magole katika barabara kuu ya Morogoro -Dodoma ambalo sehemu kubwa ya udongo uliokuwa kwenye kingo zake imezolewa maji litakamlika ndani ya siku chache zijazo iwapo hakutatokea mafuriko mengine katika eneo hilo.
