Waziri wa uchukuzi Mh,Dr.Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwakwe Jijini Dar Ea Salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na wizara ya Uchukuzi kuhusu sakata la madawa ya kulenya yaliokamatwa huko Afrika Ya Kusini hivi karibuni
Serekali imetangaza kuwafukuza kazi wafanya kazi watano wa mamlaka ya viwanja vya ndege na kuwafungulia mashtaka ya jinai chini ya sheria ya kuzuia madawa ya kulevya wafanya kazi hap wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa tuhuma za kuhusika na njama za kupitisha mabegi tisa ya kilo 180 ya dawa za kulenya ambayo yalikamatwa nchini Afrika Ya Kusini julai tano mwaka huu.
Mh, Dr.Harrison Mwakyembe akiwaonyesha waandishi wa habari Picha ya moja ya Msichana Agness Gerald (masogange) aliyekamatwa na madawa hayo huko Afrika Ya kusini hivi karibuni
Wazir wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe amewaeleza waandishi wa habari Jijini dar es Salaam kuwa, wizara hiyo imeliagiza jeshi la polisikumuondoa mara moja kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Askari polisi Coplo Ernest na kumchukulia hatua za kinidhamu askari huyokwa kushiriki kwake kwa njia moja ama nyingine na njama za kupitisha mabegi hayo yaliokuwa na dawa za kulenya, Sambamba na kuitaka idara ya usalama wa taifa kuendesha kuendesha uchunguzi wa kina kwa maafisawake waliokuwa zamu siku ya tukio kwa kuchelewesha kufikisha Mbwa kwa wakati na hivyo kushindwa kufanya ukaguzi wa kina wa mabegi hayo.
Uamuzi huo wa wizara ya uchukuzi umefikiwa baada ya uchunguzi wa Kamera za ulinzi zilizokua zikionyesha baadhi ya wafanya kazi hao walivyokuwa wakishiriki kuhakikisha mabegi hayo tisa yaliokuwa yakifanana yakibebwa na Agness Gerald Deal maarufu kama masogangena Melisa Edward yanapita kwenye uwanja huo.
Uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Mwl. Nyerere umekuwa ukitumiwa na wasafirishaji wa dawa za kulevya kupitisha mizigo yao na hivyo kuliletea taifa aibu kwenye medani ya kimataifa