Rais Jakaya Kikwete amesema serikali iko
katika hatua za mwisho kukamilisha sera ya gesi asilia na kuiwasilisha bunge hivi karibuni itayoangalia zaidi manufaa kwa taifa, mazingira ya ushiriki wa watanzania sambamba na mpango wake wa kuwezesha sekta binafsi kwa uchumi wa nchi na watu wake.
Raisi Dk. Kikwete amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa 19 wa watafiti wa masuala ya uchumi ulioandaliwa na taasisi inayo jishughulisha na masuala ya utafiti wa kiuchumi na kupunguza umaskini nchini Repoa akieleza kuamini hatua hiyo kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kupambana na kupunguza umaskni.
Awali akitoa ufafanuzi wa malengo ya mkutano huo mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Repoa Prof. Samweli Wangwe pamoja na kueleza umuhimu watanzania wote kushiriki katika uchumi amesema mkutano huo umejumuishaa wataalamu na watafiti wa uchumi kupitia viwanda na kilimo ambao watajadili kwa muda wa siku mbili na kutoa mapendekezo kwa serikali, nchi wahisani pamoja na jumuia za kimataifa katika masuala ya upatikanaji wa ajira na uchumi kwa manufaa ya watanzania.