Serikali ya Uingereza imeahidi kuboresha maeneo yote hatarishi katika Manispaa ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam ambayo yamekumbana na zoezi la bomoa bomoa.
Ahadi hiyo imetolewa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, PAUL MAKONDA.
Baada ya kumpokea Balozi huyo, na kumweleza changamoto zinazoikabili Manispaa yake, mkuu wa wilaya hiyo akaeleza mpango uliowekwa na Serikali ya Uingereza kusaidia kuboresha maeneo hatarishi ndani ya Manispaa ya Kinondoni.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni, ameomba Manispaa yake kusaidiwa Kompyuta 1,600 zitakazotumika katika Shule mbalimbli, pamoja na Magari 34 ya kubebea Wagonjwa.