Katika watu wanaovuta ukiweka top 20 ya best smokers in the world, Snoop Doggy hawezi kukosekana akifuatiwa na cousin yake Wiz Khalifa.
Snoop Doogy kwa sasa anajiita Snoop Lion alifunguka khuhusu siku aliyovuta akiwa White House alifunguka hayo wakati Jimmy Kimmel.
Aliulizwa umeshawahi kuvuta ndani ya White House.
“Bafuni, sio White House, lakini bafuni, niliuliza naweza kutumia bafu mara moja, akaniuliza naenda kufanya nini? Namba 1 au Namba 2, Nilisema namba 2, kama kawaida huwa na kuwa na sigara na kiberiti, nawasha alafu napuliza uturi kuondoa harufu , Wakaniambia unaweza ukachoma kipande cha kitambaa, nikawaambia nitafanya hivyo, na kitambaa hicho kilikuwa hiki” alisema Snoop Dogg huku akivuta akielezea experience yake ya kuvuta akiwa White House.
Wakati kipindi kikiendelea Kimmel alimtania Snoopy kwamba ABC hawaruhusu wageni kuvuta kwenye kipindi kama alivyokuwa akifanya Snoopy wakati kipindi kikwa hewani lakini alikuwa akimtania tu!!
Snoop Doggy alikuwa akimsupport Rais Obama kwa miaka mingi, mwaka 2012 alimpigia kura Obama.