
Ni miezi nane toka Soulja Boy alipokamatwa kwa kuendesha gari ikiwa imebeba bunduki kinyume cha sheria pamoja na bangi na sasa kesi hiyo ndo imefunguliwa rasmi.
Taarifa za TMZ zimeeleza kwamba msanii huyo kutoka Chicago alishtakiwa kwa kukutwa na bunduki na bangi kwenye gari yake kwenye tukio hilo la mwezi Januari, alisimamishwa ghafla na polisi Los Angeles ndipo alipokutwa na vitu hivyo.
Kufuatiwa kusachiwa gari yake alikutwa amebeba 38 caliber Smith & Wesson revolver na bangi.
Bunduki ilikutwa kwenye chini ya kiti cha gari aina ya Porsche Panamera aliyokuwa akiendesha.
Soulja Boy anasema ilikuwa ni gari ya jirani yake na ndiye aliyeiweka bunduki hiyo, Hakuna neno lolote lililotolewa kwanini polisi wa Los Angeles wamechukua muda mrefu sana kufungua kesi hiyo.
