Marion Suge Knight aliripotiwa kupelekwa hospitali ambapo alifanyiwa upasuaji baada ya kupigwa risasi zaidi ya moja, Taarifa za polisi wanasema kwa sasa wanachunguza kilichosababisha, familia ya Suge Knight imeeleza kupitia TMZ.
Suge Knight alipigwa risasi mara mbili kati ya saa 7:30 usiku jana Agosti 24 huko kwenye club ya usiku inayoitwa 1-OAK magharibi mwa Hoolywood California.
Shahidi mmoja ameeleza kuwa Chriss Brown alikuwa akisimamia tukio hilo kama MC akiwa na mwanamitindo Tyson Beckford na Black Eyed Peas Apple de Ap wanasema walisikia milio ya risasi mara nne kwenye club hiyo ya asubuhi.
Suge Knight anafahamika kwa kazi zake akiwa CEo wa Death Row Records, alifanikiwa kutoka nje ya club peke yake ripoti imeeleza ndipo polisi wakamsaidia kumuingiza kwenye gari la kubeba wagonjwa ambulance.
Knight ni mmoja ya watu watatu waliopigwa risasi, kutokana na vyombo vya habari, na mmoja wao yuko katika hali mbaya, TMZ pia imeripoti kwamba askari wakati wapo hapo watu waliokuwa ndani ya club walitoka mikono yao ikiwa juu baada ya kupigwa risasi hizo.
Game ameripotiwa kuhusika kwenye ugomvi huo na walinzi wa club hiyo mapema jioni ile, haipo wazi kama matukio hayo mawili yanauhusiano.